Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 04, 2022 Local time: 01:16

Marekani yasema hali Sudan inatisha


Marekani yasema hali Sudan inatisha
<!-- IMAGE -->

Balozi wa Marekani kwa Umoja wa Mataifa, Susan Rice, anasema hali ya Sudan inatisha wakati nchi hiyo ikijiandaa kwa uchaguzi wa kitaifa.

Susan Rice aliwaambia waandishi wa habari baada ya mkutano mfupi wa faragha na mkuu wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa, Alain Le Roy, Jumatano kwamba kuna njama kubwa katika harakati za uchaguzi na kwamba huo ni wasi wasi mkuu.

Balozi Rice alisema kuna fitina ikiwemo kuwekewa masharti kwa wanaharakati, kubughudhiwa kwa vyombo vya habari na kunyimwa haki kwenye vituo vya kupigia kura.

XS
SM
MD
LG