Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 05:58

Upinzani unachukua madaraka Krygyzstan


<!-- IMAGE -->

Marekani imelaani mgogoro wa kisiasa na ghasia zilizoikumba nchi ya Krygystan na kuomba serikali na upinzani kuingia katika meza ya majadiliano. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani inasema inaelewa kuwa serikali ya Bishkek ya Rais Kurmanbek Bakiyev ingali inafanya kazi licha ya madai kuwa rais huyo amejiuzulu.

Kwa muda mrefu Marekani imeikosoa serikali ya Kyrygstan kutokana na rekodi yake mbaya ya haki za binadamu.Lakini serikali ya Bakiyev imekuwa mshirika mkuu kwa jeshi la Marekani kwa kutoa viwanja vyake kutumiwa na majeshi ya Marekani huko Afghanistan.Hivyo basi maafisa wa Marekani wanasihi pande zote mbili kutatua mgogoro wao wa kisiasa kwa njia ya amani.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, P.J. Crowley, anasema Marekani inafuatilia kwa karibu matukio ya mjini Bishkek na inatoa mwito wa uchunguzi kamili na uwajibikaji wa kisheria kwa vifo vyovyote na matukio mengine ya manyanyaso yaliyotokea nchini humo.

Crowley anasema ujumbe wa ngazi ya juu wa serikali ya Krygystan unakuja Washington kwa ziara iliyopangwa hapo awali, unaojumuisha waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Kanat Saudabayev, na Maxim Bakiyev mtoto wa kiume wa rais wa nchi hiyo na kwamba mazungumzo baina yao na maafisa wa serikali ya Marekani yataendelea ingawaje sasa yameahirishwa hadi ijumaa kufuatia ghasia zilizotokea Bishkek.

Anasema kituo cha kijeshi cha Manas kaskazini mwa Krygystan karibu na mji mkuu wa Bishek kinaendelea kuhudumia ndege za Marekani kutoka Afghanistan na kwamba Ubalozi wa Marekani nchini humo unaendelea na shughuli zake kama kawaida.

XS
SM
MD
LG