Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 07, 2023 Local time: 01:54

Upinzani Comoros unailaumu Tanzania kwa upendeleo


Upinzani Comoros unailaumu Tanzania kwa upendeleo

Viongozi wa upinzani wa visiwa vya Comoros wanailaumu Tanzania kwa kuipendelea serikali ya Rais Abdallah Sambi, licha ya kwamba imekiuka katiba ya nchi kwa kuliruhusu bunge kuongeza muda wa muhula wa rais.

Msemaji wa mungano wa vyama vya upinzani Ali Houmed Msaidie, alitoa malalamiko hayo baada ya waziri wa mambo ya nchi za nje wa Tanzania Bernard Membe kuvitembelea visiwa hivyo bila ya kukutana na vyama vya upinzani wiki hii.

Msaidie anasema, ili bidi waziri Membe ajaribu kutanzua mzozo uliyopo visiwani humo kutokana na bunge jipya la Comoro kuidhinisha mabadiliko ya katiba na kuongeza muda wa muhula wa raia Ahmed Abdalah Sambi kwa miezi 18. Badala yake ansema waziri Membe alitoa matamshi ya kuzidisha mvutano, na bila hata kukitembelea kisiwa cha Mwali kutathmini hali ya mambo huko.

<!-- IMAGE -->

Kufuatana na msemaji wa upinzani ni kwamba bunge halina mamlaka ya kisheria kuongeza muda wa mhula wa rais.

Viongozi wa Upinzani wanasema wamesikitishwa na kushangazwa na msimamo wa Tanzana wa kuingilia kati mzozo wa Comoros na kupendelea upande moja, kutokana na matamshi ya bw Membe, wakati wanafahamu kwamba daima Tanzania hujaribu kusaidia kutanzua mizozo ya visiwa hivyo bila ya kupenelea upande wowote.

Msemaji wa upinzani Bw Msaidie amesema upinzani utaipelekea serikali ya Tanzania malalamiko rasmi Jumatano, kutokana na matamshi ya waziri wa mambo ya kigeni yanatofautiana na yale ya Rais Jakaya Kikwete, alipowambia wakomoro mwaka jana kwamba tanzania haitounga mkono kamwe kiongozi yeyote atakae badilisha kaika kwa maslahi yake binafsi.

XS
SM
MD
LG