Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 26, 2023 Local time: 04:46

Mbunge wa CCM akanusha kuwepo makundi bungeni


Mbunge wa CCM akanusha kuwepo makundi bungeni
<!-- IMAGE -->

Mbunge wa jimbo la Kahama mkoani Shinyanga James Lembeli amekanusha taarifa iliyotolewa na gazeti la Mwananchi, likimkariri akisema kuwa kuna kundi la mafisadi ndani ya CCM wanaotaka kumwondoa katika chama hicho.

Akizungumza na sauti ya Amerika mbunge huyo wa chama tawala alisema “nilichokisema ni kuwa kuna watu sasa hao watu, kwa jinsi ambavyo katika miezi ya karibuni kumekuwa na maneno maneno, hawa watu sidhani kuwa wana nia njema na mimi na wenzangu wanaopambana na ufisadi na anayehusika sijui ana sababu gani za msingi.”

Kuhusu hali ya kuwepo makundi ndani ya bunge Bw.Lembeli anasema tangu achaguliwe kuwa mbunge hajashuhudia kundi rasmi bungeni isipokuwa unapotoa wazo au hoja na wabunge wengine wakakuunga mkono mara moja mnatajwa kuwa ni kundi hili au kundi lile, na ikiwa kuna kundi rasmi basi anatoa hoja si kungelikuwepo na msemaji wake na maafisa wengine?

Akizungumzia kujiondoa kwa mwenzake aliyekuwa mbunge wa Kishapu Richard Mpendazoe, mbunge huyo wa Kahama hakutaka kutoa maoni yake hata hivyo anasema kuweza kuushinda ulaji rushwa na ufisadi ndani ya CCM ni kupambana ndani ya chama na wala sio nje akidai kwamba “nitakufa kama mwanachama wa CCM”.

XS
SM
MD
LG