Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 11:43

Wabunge Kenya wakubali rasimu ya katiba


Wabunge Kenya wakubali rasimu ya katiba
<!-- IMAGE -->

Wabunge wa Kenya wamekubali rasimu mpya ya katiba ambayo itapigiwa kura ya maoni baadae mwaka huu. Bunge lilikubali rasimu hiyo Alhamisi.

Wabunge walipendekeza zaidi ya vipengele 100, lakini vilishindwa kupitishwa katika mabadiliko yaliyopendekezwa wakati wa mjadala huo. Rasimu ya katiba imeundwa kupunguza madaraka kwa Rais na kudhibiti utumiaji mbaya wa madaraka.

Hii itakuwa sehemu ya marekebisho yaliyopendekezwa katika mkataba wa kushirikiana madaraka kati ya Rais Mwai Kibaki na mpinzani wa zamani Raila Odinga, baada ya uchaguzi mkuu uliokuwa na utata na kusababisha mapigano nchini humo miaka miwili iliyopita.

XS
SM
MD
LG