Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 13:49

Japani inaipatia kenya mkopo wa dola milioni 300


Japani inaipatia kenya mkopo wa dola milioni 300
Japani inaipatia kenya mkopo wa dola milioni 300
<!-- IMAGE -->

Kenya imetia saini mkataba wa mkopo wa zaidi ya dola milioni 300 kutoka Japan, ili kupanua mitambo ya nishati katika mkoa wa Rift Valley.

Maafisa wanasema mkopo huo wa fedha utasaidia ujenzi wa vituo viwili vipya katika kiwanda cha nishati huko Olkaria. Vituo hivyo vitasambaza megawati 140 za umeme wa ziada. Maafisa wa Kenya walitangaza mkataba huo Jumatano.

Waziri wa fedha Uhuru Kenyatta, anasema bei kubwa ya mafuta na tegemezi zaidi la umeme lilichochea Kenya kuvigawa vyanzo vyake vya nishati.

XS
SM
MD
LG