Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 02:10

Mvutano wa kisiasa katika uchaguzi wa Sudan


Mvutano wa kisiasa katika uchaguzi wa Sudan
Mvutano wa kisiasa katika uchaguzi wa Sudan

<!-- IMAGE -->

Rais wa Sudan Omar al-Bashir anaonya ikiwa waasi wa zamani wa Sudan ya Kusini watasusia uchaguzi mkuu wa kitaifa mwezi ujao , upande wa kaskazini nao hautaendelea na kura ya maoni ya kuamua juu ya kujitenga kwa upande wa kusini.

Bwana Bashir aliuambia mkutano mjini Khartoum kwamba ikiwa chama tawala cha Sudan ya Kusini, Sudan People’s Liberation Movement-SPLM, kitakataa kushiriki katika uchaguzi mkuu basi nao watakataa kushiriki katika kura ya maoni. Lakini SPLM walisema mapema jana wapo tayari kushiriki katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi nchini humo tangu mwaka 1986.

Akizungumza na waandishi wa habari huko Juba, naibu katibu mkuu wa chama cha SPLM, Anne Itto, alisema chama chake hakijawahi kuunga mkono wito huo kutoka vyama vya upinzani vya kaskazini kuchelewesha upigaji kura uliopangwa kufanyika mwezi April.

Uchaguzi huo ni sehemu kuu ya mkataba wa amani wa mwaka 2005 ambao ulimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Sudan kusini na kaskazini.


XS
SM
MD
LG