Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 12:55

Uganda haina nia ya kurudisha majeshi Congo


Uganda haina nia ya kurudisha majeshi Congo
Uganda haina nia ya kurudisha majeshi Congo
<!-- IMAGE -->

Uganda imekanusha ripoti ya baadhi ya vyombo vya habari kuwa huenda jeshi la Uganda likarudi mashariki mwa Congo kupambana na waasi wa LRA ikiwa serikali ya Kinshasa itahitaji.

Akizungumza na Sauti ya Amerika Msemaji wa jeshi la Uganda Luteni kanali Felix Kulayigye amekanusha habari hizo na kusema kuwa jeshi lake linafanya operesheni huko Afrika ya Kati ambako wanaamini kuwa Kony na kundi lake la waasi wa LRA bado wako huko.

Akielezea mafanikio ya operesheni hiyo amedai kuwa wamekamta na kuuwa makamanda wengi wa LRA halikadhalika wameokoa wanawake wengi waliokuwa wakibakwa na watoto waliolazimishwa kuwa wapiganaji.

Akiulizwa juu ya kwanini hawakuweza kuwashinda mara ya kwanza walipowashambulia LRA na kutangaza ushindi mkubwa hapo Disemba 2008.

Luteni kanali Kulayigye, alisema anashangaa kwamba hilo lingali ni suala linaloulizwa, anasema “ulimwengu mzima waasi huwa wanachukua muda kumaliziwa hasa hasa ikiwa wanaepuka au wanajificha jinsi LRA wanavyofanya".

Na “nikitoa mfano, ukiangalia vita vya Angola, vita vya IRA kati ya Uingereza na Northern Ireland, ukitizama vita dhidi ya mgaidi Osama bin Laden, ambae sasa hivi anatafutwa na nchi 43, vyote hivyo vinachukua muda mrefu”.

Matamshi hayo yanatokana na tuhuma za kundi la kutetea haki za binadam, Human Rights Watch mwishoni mwa wiki kwamba LRA waliwauwa wakazi 321 katika vijiji 10 kaskazini mashariki ya DRC mwezi Disemba 2009, lakini haikuripotiwa hadi hivi sasa. Jeshi la Uganda haijakubaliana na ripoti hiyo ya HRW.

XS
SM
MD
LG