Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 02:27

Zaidi ya watu 300 wagunduliwa kuuwawa DRC


Zaidi ya watu 300 wagunduliwa kuuwawa DRC
Zaidi ya watu 300 wagunduliwa kuuwawa DRC
<!-- IMAGE -->

Kundi moja la kutetea haki za binadamu linasema waasi huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo waliwauwa wanavijiji wasiopungua 321 katika mauaji yasiyoripotiwa, mwanzoni mwa Disemba mwaka jana.

Katika ripoti iliyotolewa jumapili, kundi hilo Human Rights Watch linasema waasi wa kundi la Lord’s Resistance Army kutoka Uganda walivamia vijiji visivyopungua 10 katika siku nne za mapigano huko kaskazini-mashariki mwa eneo la Makombo nchini DRC.

Kundi hilo linasema wanavijiji wengi waliouwawa ni wanaume ambao walifungwa kamba na kuuwawa kwa kukatwa mapanga. Kundi hilo linasema vifo hivyo vilijumuisha wanawake 13, na watoto 23, akiwemo msichana wa miaka 3 ambaye alichomwa moto hadi kufa.

Human Rights Watch linasema waasi wa LRA wamewateka nyara zaidi ya watu 250 kutoka vijiji hivyo wakiwemo watoto 80.Linasema kinyume na inavyoashiriwa na serikali za Uganda na DRC, kundi la LRA bado ni tishio kubwa.

XS
SM
MD
LG