Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 23:29

Vatikan yalaumu vyombo vya habari


Vatikan yalaumu vyombo vya habari
Vatikan yalaumu vyombo vya habari
<!-- IMAGE -->

Vatican imelaumu vyombo vya habari kufuatia ripoti kuwa wakati Papa Benedict alipokuwa Kardinali alishindwa kuchukua hatua dhidi ya Padri mmoja wa Marekani aliyeshutumiwa kwa kuwalawiti watoto wa kiume wapatao 200.

Tahariri ya gazeti la Vatican L’Osservatore Romano leo ilisema kuwa hakukuwa na kificho chochote kuhusiana na kesi ya Padri Lawrence Murphy. Iliita jaribio hilo kuwa ni jaribio lisilo na msingi la shutuma za kumkandamiza Papa Benedict kwa kutumia kila njia iwezekanyo.

Makala hayo yalitetea jinsi Papa alivyoshughulikia kashfa hiyo ya ngono ndani ya kanisa katoliki ikiwa imewekwa kwa uwazi, uthabiti na kwa hali ya juu.

XS
SM
MD
LG