Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 26, 2022 Local time: 23:20

Ajali nyingine yaua 11 Tanzania


Ajali nyingine yaua 11 Tanzania
<!-- IMAGE -->

Inakadiriwa watu 11 wamefariki dunia katika ajali mbaya ya gari kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka saba mjini Dar es salaam, Tanzania Jumatano Alfajiri.

Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi wa kikosi cha usalama barabarani Bw. Mohamed Mpinga amesema ajali hiyo ilitokea katika eneo la Kibamba CCM katika wilaya ya Kinondoni baada ya Lori la mafuta kugonga gari dogo la abiria aina ya Toyota, Hiace.

Hata hivyo kamanda huyo amesema ameshindwa kutoa idadi kamili katika ajali hiyo kwani watu wote katika basi hilo dogo walifariki na maiti zao hazikuweza kutambulikana kutokana na jinsi zilivyoharibika kwa kukatika viungo.

Kamanda huyo wa Polisi ameahidi kutoa idadi kamili baadae mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Walioshuhudia wanasema ajali hiyo huenda imetoka na gari kwenda kasi kupita kiasi na serikali ya Tanzania imeanzisha juhudi ya kupambana na ajali barabarani kwa kurudisha mpango wa kuweka vidhibiti mwendo.

XS
SM
MD
LG