Kaimu rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameteuwa watu 33 katika baraza lake la mawaziri ikiwemo binamu wa kiume wa rais anayeugua Umaru Yar’Adua.
Rais wa baraza la seneti alisoma majina ya watu hao leo bila kutaja uwezekano wa nyadhifa zao.
Orodha hiyo pia ina majina ya mawaziri tisa waliokuwemo katika baraza la zamani akiwemo waziri wa habari wa zamani Dora Akunyili mfuasi mkuu wa bwana jonathan.
Watu wapya ni pamoja na Olusegun Aganga mkurugenzi mkuu wa shirika la kifedha la Goldman Sachs lenye makao yake mjini London , na Mutallab Yar’Adua binamu yake rais.
Rais Yar’Adua kimsingi bado yuko madarakani lakini hajaonekana hadharani tangu alipougua sana mwishoni mwa novemba mwaka jana. Bunge lilimteua makamu rais jonathan kuwa kaimu kiongozi wa nchi wiki sita zilizopita.