Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 10:02

Obama Asaini Mswaada wa Afya


Rais Obama ametia saini kuwa sheria mswaada wa mageuzi ya huduma za afya nchini Marekani katika sherehe fupi zilizofanyika katika ikulu ya Washington. Mswaada huo ni mkubwa kuliko yote katika huduma za jamii tangu mswaada wa huduma za ustawi wa jamii uliopitishwa miaka 40 iliyopita.

Akipigiwa makofi na wanaomwunga mkono Rais Obama alisema " Leo baada ya karibu karne nzima ya kujaribu, leo, baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa mijadala, leo, baada ya kura zote kuhesabiwa, mageuzi ya huduma za afya yanakuwa sheria nchini Marekani."

Rais alisema ana imani kuwa baraza la seneti litaboresha mageuzi hayo haraka iwezekanavyo. Alisema baadhi ya sheria zitaanza kazi mara moja na nyingine zitachukua muda kidogo.

XS
SM
MD
LG