Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 11:42

Tanzania na Zambia wakataliwa uuzaji pembe za Ndovu


Kundi moja la Umoja wa Mataifa limekataa maombi kutoka Tanzania na Zambia kufanya mauzo ya mara moja ya pembe za ndovu. Taarifa hiyo ilitolewa Jumatatu kwenye mkutano wa mataifa 175 unaozungumzia biashara ya kimataifa huko Doha, Qatar.

Biashara hiyo ingelikiuka marufuku ya kitaifa iliyowekwa mwaka 1989 juu ya uuzaji wa pembe za ndovu ili kuwalinda tembo kutokana na uwindaji haramu. Jason Bell-Leask, afisa wa mfuko wa kimataifa wa wanyama pori alisema tamko hilo ni ushindi nadra kwa tembo.

Tanzania na Zambia walisema idadi ya tembo wao imeongezeka kufikia kiwango ambacho wanaharibu mazao na kuuwa watu. Wapinzani walisema nchi hizi mbili zimeshindwa kuzuia uwindaji haramu wa tembo na uuzaji haramu wa pembe za ndovu.

Tanzania iliomba kibali cha kuuza hifadhi iliyopo ya pembe za ndovu zenye thamani ya dola milioni 20. Zambia pia iliomba ombi kama hilo kisha ilijitoa na kupendekeza uuzaji wa sehemu zingine za tembo.


XS
SM
MD
LG