Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 03:57

Nigeria yakasirishwa na matamshi ya Gadhafi


Serikali ya NIgeria imemuita nyumbani balozi wake huko Tripoli baada ya kiongozi wa Libya Muammar Gadhafi kupendekeza kwamba taifa hilo ligawanywe na kuwa mataifa mawili. Taifa la kiislam na taifa la kikristo kama suluhisho la kukabiliana na ghasia za kidini na kikabila.

Matamshi ya kiongozi huyo wa Libya aliyoyatoa wakati wa mkutano na wanafunzi wa kiafrika huko Tripoli siku ya Jumanne, yamesababisha majibu makali na ya hasira kutoka serikali ya Abuja.

Wabunge wa Nigeria walilaani matamshi ya Gadhafi wakati wa mjadala wao bungeni. Rais wa baraza la seneti David Mark alisuta matamshi ya kiongozi wa Libya na kuyaeleza kama uropokaji wa mwendawazimu.

Serikali ya Nigeria inasema kwamba kumrudisha balozi wake nyumbani ni sehemu ya kutathmini uhusiano wake na Libya, lakini ilifafanua kwamba haifiki kiwango cha kuvunja uhusiano wa kidiplomasia.

Katika pendekezo lake bwana Gadhafi alisema kwamba upande wa Kusini liwe taifa la wakristo na mji mkuu wake wa Lagos na upande wa kaskazini liwe taifa la waislam na mji mkuu wake Abuja. Nigeria ambayo inawakazi milioni 140 imegawanyika kati ya waislam na wakristo.

XS
SM
MD
LG