Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 04:40

Mahakama ya kimataifa yapinga rufaa ya Bikindi


Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita inayosikiliza kesi za watuhumiwa wa Rwanda imeshikilia msimamo wake wa awali wa kifungo cha miaka 15 jela dhidi ya mwanamuziki Simon Bikindi.

Mnamo Desemba mwaka 2008 mahakama ilimkuta na hatia ya uchochezi wa mauaji ya halaiki mwanamuziki huyo kufuatia hotuba aliyoitoa Juni mwaka wa 1994 alipowasihi wahutu kujihami na kuwauwa watu wa kabila la watutsi.

Bikindi alikata rufaa dhidi ya hukumu hiyo lakini mahakama ikapinga tetesi zake Alhamisi. Hata hivyo majaji walisema watahesabu miaka ambayo mwanamuziki huyo ameshikiliwa tangu alipokamatwa mwezi Julai mwaka 2001.

Bikindi anafahamika vyema Rwanda kwa nyimbo kadhaa alizotunga zikiwalaumu watu wa kabila la Watutsi kwa matatizo ya Rwanda na kuwaelezea kama maadui. Baadhi ya nyimbo zake zilichezwa katika radio ya taifa ya Rwanda miezi kadhaa kabla ya mauaji ya halaiki ya mwaka 1994.

XS
SM
MD
LG