Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 09:48

Wataalamu wa ukimwi eneo la IGAD wakutana Kenya


Wataalamu wa ugonjwa wa ukimwi katika mataifa wanachama wa shirika la maendeleo pembe ya Afrika-IGAD wanakutana mjini Nairobi nchini Kenya kutathmini madhara yanayosababishwa na kuenea kwa ugonjwa huo katika eneo hilo la Afrika. Wataalamu hao wanachunguza mikakati mipya kuwahudumia waathiriwa wa ugonjwa huo hasa wakimbizi, wafugaji wa kuhama hama pamoja na madereva wa magari ya masafa marefu.

Hii ni mara ya kwanza kwa wataalamu hao wa ugonjwa wa ukimwi katika mataifa wanachama wa shirika la IGAD, kushauriana kwa pamoja kuhusu tatizo hili la ugonjwa wa ukimwi katika eneo hili la Afrika ambalo katika siku za hivi karibuni limekuwa ni tatizo sugu kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wakimbizi hasa kwenye mipaka ya Kenya, Uganda, Somalia na maeneo ya kusini mwa Sudan.

Kutokana na kuenea kwa ugonjwa huu wa ukimwi katika mataifa haya ya IGAD, kitengo maalumu kimeanzishwa na wataalamu wa ugonjwa huo kwa lengo la kujenga zahanati na kutoa matibabu kwenye sehemu za mpakani na kwenye kambi za wakimbizi.

Wataalamu hao wanasema wakati raia wa sehemu moja wanasafiri na kuhama sehemu moja hadi nyingine wakati mwingine wanaeneza magonjwa ya kuambukiza ambao waliambukizwa katika makazi yao ya zamani.

XS
SM
MD
LG