Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 14:42

Jacob Zuma awasili Zimbabwe kutatua mzozo wa kisiasa


Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amewasili Zimbabwe Jumanne ili kujaribu kuondoa mkwamo wa kisiasa katika serikali ya umoja wa kitaifa iliyoundwa mwaka mmoja uliopita.

Bw. Zuma anakwenda akiwa kama msuluhishi wa SADC. Ofisi yake imesema itaangalia njia jinsi gani mpango huo wa kushirikiana madaraka utatekelezwa na kuangalia njia za kupelekea haraka hatua hiyo.

Bw.Zuma anapanga kufanya mikutano na Rais Robert Mugabe na waziri mkuu Morgan Tsangirai ambao waliingia katika serikali ya umoja baada ya mzozo na ghasia za kupinga uchaguzi zilizogubika uchaguzi wa 2008.

XS
SM
MD
LG