Shirika la kimataifa la uhamiaji - IOM - linasema karibu watu millioni mbili waliokoseshwa makazi wakati wa vita vya kusini mwa Sudan sasa wamerejea nyumbani tangu kutiwa saini mkataba wa amani 2005.
IOM inasema karibu nusu ya watu hao wamerejea katika maeneo ambayo waliyakimbia na kuongeza kuwa idadi kubwa ilirudi kaskazini mwa jimbo la Bahr el Ghazal na kusini mwa Kordofan. Msemaji wa IOM Jean Philippe Chauzy alisema kuwa idadi ya waliorejea ilikuwa kubwa zaidi kati ya mwaka 2006 na 2007 wakati robo tatu ya watu millioni moja waliporejea kila mwaka kusini mwa Sudan.
Hata hivyo, IOM inasema wakimbizi hao wengi waliorudi wanakabiliwa na changamoto zisizo za kawaida hasa katika mahitaji ya msingi kama vile maji safi, chakula, huduma za afya na kazi.