Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 03:30

Ukarabati wa barabara ya Uganda na Rwanda waanza


Maafisa wa Uganda wanakarabati barabara kuu inayoiunganisha nchi hiyo na Rwanda, baada ya mvua kubwa kuharibu sehemu ya barabara hiyo.

Maafisa kwa muda wamezuia magari makubwa na mabasi kutumia barabara hiyo, ambayo inaunganisha mji wa Uganda wa kabala na mji wa mpakani huko Rwanda wa katuna.

Sehemu ya barabara imedidimia ardhini mapema wiki hii. Mamlaka ya taifa ya barabara nchini Uganda imesema hali hiyo ni ya dharura na imepeleka wahandisi na vifaa kuitengeneza barabara hiyo.

XS
SM
MD
LG