Changamoto zilizosalia ni kubwa,lakini mwezi mmoja kabla ya upigaji kura kuanza, baraza la amani na usalama la umoja wa afrika linasema, uchaguzi wa rais na wa bunge nchini sudan una nafasi nzuri ya kufanikiwa.
Tathmini imefanyika baada ya baraza kusikiliza maoni ya jopo ambalo hivi karibuni lilitembelea mikoa yote, ikiwa ni pamoja na eneo lililokumbwa na ghasia la Darfur, na vilevile eneo la kusini lenye utajiri wa mafuta, ambalo linatazamia kuitisha kura ya maoni kuhusu uhuru wao mwezi January mwaka ujao.
Balozi wa Zambia kwenye umoja wa Afrika, Albert Muchanga, ambaye hivi sasa ni rais wa baraza hilo, anasema wanachama wana wasiwasi kuhusu kile alichokiita pengo kwenye masuala kama vile ya usalama.
Aliwaambia waandishi habari kuwa mambo mengi yanategemea mikataba miwili ya hivi karibuni, sitisho la mapigano kati ya serikali ya Khartoum na kundi kubwa la waasi huko Darfur, na vile vile kanuni za uchaguzi.
Alisema “Kila mtu ameona mapengo, na kuashiria kusonga mbele ili kuziba mapengo hayo. Bora tulenge mikataba miwili ambayo tayari imetiwa saini. Kile ambacho kinatutia wasi wasi ni kama mikataba hiyo itatekelezwa.”
Hatua nyingine muhimu itatokea katika mji mkuu wa Qatar, huko Doha, ambako wasuluhishi wanajaribu kupanua mkataba uliotiwa saini hivi karibuni huko Darfur wa kusitisha mapigano ili ujumuishe makundi ambayo hayajatia saini.
Naibu balozi wa sudan kwenye umoja wa afrika, Akuie Bona Malwal, anasema macho yote yatamulika Doha kwa makubaliano ambayo yatahakikisha kuwa sitisho la mapigano linawahusu wote huko Darfur.
Alisema “Inategemea nini kitatokea huko Doha. Ikiwa watatia saini kesho, basi wataweza kuruhusiwa kushiriki, na ni huko Darfur Magharibi tu, ambapo kuna ukosefu wa mkubwa wa usalama.
Makundi mengi ya Darfur yako tayari kushiriki,kwa hiyo hivi sasa utasema vipi kuwa ni uchaguzi wa wote huko Darfur, kwa sababu ni idadi ndogo tu ndiyo itashiriki katika uchaguzi,lakini hilo linategemea matokeo ya doha.