Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 14, 2024 Local time: 23:16

Afisa wa Marekani aomba msamaha kwa Libya


Afisa wa Marekani ameomba msamaha kwa matamshi aliyotoa na kuonekana kuwa ni shambulizi kwa kiongozi wa Libya Muamar Gadhafi.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje P.J.Crowley anasema matamshi yake kuhusu Bw.Gadhafi kutaka kuwepo kwa jihad au vita vitakatifu, dhidi ya Uswizi haiashirii sera ya Marekani na wala haikuwa na azma ya kuleta ubishani.

Crowley anasema anasikitika kwamba matamshi yake yamekuwa ni kikwazo kwa uhusiano wa Marekani na Libya.

Anasema waziri mdogo wa mambo ya nje Jeffrey Feltman atakwenda Tripoli wiki ijayo kwa mazungumzo kati ya nchi hizo mbili.

XS
SM
MD
LG