Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 25, 2024 Local time: 15:32

Matukio ya Upigaji majumbani yaongezeka Kenya


Makund i ya haki za binadamu na huduma za afya Kenya yanaripoti ongezeko la kesi za upigaji majumbani. Wataalam wanasema ongezeko hilo inawezekana limesababishwa na ongezeko la upigaji wenyewe au watu hawaoni tena aibu kuripoti matukio hayo majumbani. Kuishi na mume au mke anayepiga kunasababisha woga usiokwisha kwa mpigwaji.

Florence Wanjiku aliishi maisha ya namna hiyo kwa miaka 10 na mumewe, aliyekuwa na tabia ya kulewa. Anaelezea usiku mmoja wa ulevi. "Aliingia jikoni, na kuchukua mwiko na kuanza kunipiga kama vile unavyopiga mtoto mdogo. Lakini kwa bahati alinipiga kwa nguvu sana hadi ule mwiko ukavunjikia kichwani mwangu. Nilipata mishono minane (kichwani)."

Matukio yanayoripotiwa, kama ule wa Wanjiku, yanaongezeka Kenya, makundi ya huduma za afya na haki za binadamu yanasema.

Terese Omondi, meneja wa kituo kinachosaidia wanawake wanaopigwa majumbani anasema kituo hicho kinatoa huduma muhimu kwa wanawake hao. "Kuna ongezeko kubwa la idadi. Tulianza tukisaidia wanawake 299 mwaka 2006, 412 mwaka 2007 na mwaka 2008 tulisaidia wanawake wengine zaidi ya 400," anasema bi Omondi.

XS
SM
MD
LG