Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 02:26

Obama Ahimiza Bunge Kupitisha Mageuzi ya Afya


Rais Barack Obama anasema wakati umefikwa kwa bunge la Marekani kumaliza kazi yake katika mageuzi ya huduma za afya na kutoa wito kwa bunge hilo kupanga kura kuhusu swala hilo katika wiki chache zijazo.

Akizungumza Jumatano kutoka Ikulu ya Marekani, Rais Obama alisema anaamini kuwa wakati umefika kuwapa wananchi wa Marekani udhibiti kuhusu bima za afya zao. Akizungukwa na kundi la madaktari, wauguzi na madaktari wasaidizi rais Obama alisema kila hoja imetolewa katika swala hilo na sasa wakati wa kuchukua hatua umefika. Alisema hajui mswaada huo utakuwa na athari gani kisiasa, lakini anajua kuwa ni hatua inayofaa.

Rais Obama alisema wademocrat na warepublican wanakubaliana kuwa mageuzi yanahitajika na kwamba endapo hakuchukuliwi hatua yoyote, tatizo hilo litazidi kuwa baya. Alisema mswaada wa afya anaowasilisha sasa umechukua mawazo kutoka pande zote mbili.

XS
SM
MD
LG