Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 17, 2024 Local time: 15:15

Uganda yaongoza EA katika orodha ya FIFA


Uganda inaongoza nchi za Afrika Mashariki na Kati katika orodha mpya ya timu bora duniani iliyotolewa na shirikisho la kandanda duniani - FIFA - ikiwa inashika nafasi ya 74 duniani. Uganda inafuatiwa na Rwanda ambayo inashika nafasi ya 105, ikifuatiwa na Tanzania katika nafasi ya 108.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, nyumbani kwa klabu bingwa Afrika T.P. Mazembe, inashika nafasi ya 112 wakati Kenya iko katika nafasi ya 113 na Burundi inashika mkia kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati ikiwa inashikilia nafasi ya 147 duniani.

Mabingwa wa soka barani Afrika, Misri, wamedondoka kutoka katika orodha ya kumi bora baada ya kukaa humo kwa muda wa mwezi mmoja tu. Misri sasa inashika nafasi ya 17 katika orodha hiyo, ikiwa inaongoza nchi za Afrika. Spain inaendelea kushika nafasi ya kwanza, ikifuatiwa na Brazil na Uholanzi katika nafasi ya tatu.

Kumi Bora Afrika:

1. Misri (17), 2. Cameroon (20), 3. Nigeria (21), 4. Ivory Coast (22), 5. Ghana (28), 6. Algeria (32), 7. Gabon (43), 8. Burkina Faso (51), 9. Mali (54), 10. Tunisia (55). Katika mabano ni nafasi inayoshika duniani.

XS
SM
MD
LG