Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 19:19

Kenya viongozi waungana kuadhimisha mwaka wa pili


Katika kuadhimisha mwaka wa pili tangu kundwa serikali ya mungano huko Kenya Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga, walitoa mwito kwa amani na upatanishi na kujaribu kutuliza hofu juu ya uwezekano wa kuvunjika kwa serekali.

Viongozi hao wawili walihudhuria ibada katika kanisa kuu la Holy family huko Nairobi, kuadhimisha siku hiyo. Rais Kibaki akihutubia waumini alisema ilikua ni uamuzi mkubwa sana kutia saini makubaliano yaliyohitajika sana na taifa hilo wakati huo.

Bw Odinga alisema mauwaji na ghasia zilizoshuhudiwa baada ya uchaguzi ulokua na utata zisipate kuruhusiwa kutokea tena nchini humo. Alisema serekali ya mungano imefanikiwa katika mambo mengi ukichukulia hali ngumu ya kufanya kazi.

Hata hivyo upinzani huko Kenya unahisi serekali hiyo imeshindwa kabisa na jukumu lake. Akizungumza na Sauti ya Amerika mbunge wa zamani wa Nivasha, jimbo la Rifty Valley Bi Jane Kihara, amesema hakuna maendeleo yaliyopatikana wakati kuna watu elfu kumi waliopoteza makazi yao ambao bado wanaishi ndani ya makambi huko Niavasha.

Bi Kihara ambae ni mkuu wa masuala ya jinsia katika chama cha NARC anasema lengo kubwa la serekali lilikua ni kuwarudisha nyumbani waliopoteza makazi yao, lakini hadi hivi sasa imeshindwa kuleta upatanishi kati ya wakazi waliopigana.

XS
SM
MD
LG