Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 19:50

Dubai: Kiongozi wa Hamas alibanwa pumzi


Mkuu wa polisi Dubai anasema kikosi cha siri cha majasusi wa Israel, Mossad, hakina "hata aibu" kutokana na mauaji ya mwezi Januari ya kiongozi wa Hamas katika hoteli moja ya Dubai.

"Sasa nina uhakika wa asilimia 100 kwamba Mossad walihusika katika mauaji" ya Mahmoud al-Mabhouh, alisema Luteni Jenerali Dahi Khalfan Tamim. "Nilikuwa nasema asilimia 99 lakini sasa naweza kusema asilimia 100."

Al-Mabhouh, mjumbe mwanzilishi wa tawi la kijeshi la Hamas, alikutwa amekufa katika chumba chake cha hoteli Dubai Januari 20. Polisi wanaamini aliuawa usiku uliopita, na wametambulisha washukiwa 26 katika mauaji hayo.

Israel ina kawaida ya kutokanusha wala kuthibitisha tuhuma zozote katika maswala ya usalama. Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Avigdor Liberman, hata hivyo, alisema mwezi uliopita kuwa hakuna sababu yoyote nzuri ya kufikiria kuwa Mossad walihusika katika mauaji hayo.

Mapema Jumapili polisi wa Dubai walisema matokeo ya vipimo yameonyesha kuwa al-Mabhouh alipigwa sindano ya kumlaza kabla ya kubanwa pumzi.

XS
SM
MD
LG