Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 16:07

Sarkozy afanya ziara Gabon na Rwanda


Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy ameanza ziara ya mataifa mawili yenye lengo la kurekebisha uhusiano wake na Gabon na Rwanda.

Bw.Sarkozy aliwasili Gabon leo na alipokelewa na rais Ali Ben Bongo . Viongozi hao wawili baadaye walitembelea kaburi la rais wa zamani wa Gabon Omar Bongo.

Omar Bongo baba wa rais wa sasa Ali Ben Bongo alikuwa na uhusiano wa karibu na Ufaransa katika utawala wake wa miaka 42 na alikuwa akichunguzwa huko Ufaransa kuhusu
Matumizi mabaya ya fedha mpaka wakati wa kifo chake mei iliyopita.

Bwana sarkozy kesho atasafiri kwenda Rwanda kurejesha tena uhusiano wa kidiplomasia kati ya paris na Kigali baada ya kuvunjika kwa miaka mitatu.

XS
SM
MD
LG