Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 09:47

Hatimae Rais Yar'Adua amerudi nyumbani


Ndege mbili zilionekana zikitua eneo linapotua ndege za rais katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abuja JUamnne usiku, masaa machache baada ya vyanzo vya serekali kusema Rais Umaru Yar'Adua yuko njiani anarudi nyumbani kutoka Saudi Arabia.

masahhidi kwenye uwanja wa ndege walozungumza na Sauti ya Amerika wanasema gari moja la kubeba wagonjwa lilikua karibu na ndege ilipotua. Lakini hapakutolewa taarifa rasmi juu ya hali ya kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 58, aliyekua anatibiwa kutokana na ugonjwa wa moyo kwa miezi mitatu kwenye hospitali mmoja ya Saudia.

Tangu Rais Yar'Adua kuondoka Nigeria Novemba 23 amehojiwa mara moja tu kwa muda mfupi na hajaonekana hadharani. Kutokuwepo kwake kulipelkea kuzuka mzozo mkubwa wa kikatiba huko Nigeria, hadi pale bunge lilipoingia kati na kuamua kumkabidhi makamu rais Goodluck Jonathan madaraka ya uwongozi kwa muda. Baadhi ya wabunge na mawakili wamehoji ikiwa hatua hiyo inafuatana na katiba ya nchi.

XS
SM
MD
LG