Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 07:14

Ivory Coast imetangaza tume ya uchaguzi


Serikali ya Ivory Coast imetangaza tume mpya ya uchaguzi, ikiwa ni hatua muhimu kabisa katika kujaribu kutanzua mzozo wa kisiasa wa nchi hiyo. Tangazo rasmi la kundwa tume lilitolewa Ijuma na kueleza kwamba, tume itaongozwa na mjumbe wa chama cha upinzani Youssouf Bakayoko kutoka chama cha PDCI.

Vyama vya upinzani vilikata kushiriki katika serekali hadi pale rais Laurent Gagbo kurudisha tume aliyoivunja karibu wiki mbili zilizopita. Rais aliivunja tume kwa sababu anadai ilikua inawandikisha wapiga kura kinyume cha sheria.

Aliivunja pia serikali, lakini waziri mkuu Guillaume Soro kiongozi wa zamani wa waasi alitangaza serekali mpya siku ya Jumanne.

Tume mpya ya uchaguzi itakua na jukumu la kutayarisha uchaguzi wa rais ambao umeahirishwa mara saba tangu 2005.

Wachambuzi wanasema hatua hizi zote zinaonekana zimetokana na juhudi mpya za mpatanishi wa mzozowa Ivory Coast, rais Blaise Compaore wa Burkina Faso. Mapema wiki hii aliitembele Ivory Coast na kusema pande zote za mzozo zimekubaliana kuandaa uchaguzi wa rais chini ya muda wa miezi mitatu. Anasema viongozi wamekubali kufanya uchaguzi huo mwishoni mwa Aprili au mapema mwezi Mei.

Rais Laurent Ggabo alivunja serikali na tume ya uchaguzi Februari 12 wiki chache kabla ya kufanyika uchaguizi wa rais uliocheleweshwa sana.

Hatua yake hiyo ilizusha maandamano makali mitaani Jumatatu maandamano hayo yaligeuka kuwa ya maafa ya pili, huku watu wawili wakiripotiwa kuuwawa baada ya kuzozana na Polisi katika mji wa Daloa magharibi mwa nchi.Wengine kadhaa walijeruhiwa.

XS
SM
MD
LG