Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 24, 2025 Local time: 00:08

Bunge la Kenya laanza kikao kipya


Bunge la Kenya limeanza kikao kipya leo baada ya likizo ya miezi miwili huku likiwa na kazi ngumu ya kushughulikia maswala nyeti yanayokabili taifa hilo, ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa katiba mpya nchini Kenya.

Pia kuna baadhi ya wabunge wenye nia ya kuwasilisha bungeni hoja maalum ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Raila Odinga kufuatia mgogoro wa kusimamishwa kazi kwa mawaziri wawili wa serikali, hatua ambayo ilifutwa na rais Mwai Kibaki saa chache baada ya kutangazwa na Waziri Mkuu Odinga wiki mbili zilizopita.

Jumanne Rais Kibaki na Waziri Mkuu Odinga walikutana kwa mara ya kwanza mjini Nairobi tangu mgogoro huo kuzuka lakini ripoti zinasema hawakuzungumzia swala hilo hadi hapo baadaye.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG