Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 23:34

Wabunge wa Marekani Ziarani Zimbabwe


Timu ya wabunge wa Marekani imekutana na viongozi wa kisiasa wa ngazi za juu nchini Zimbabwe katika ziara ya kutathmini maendeleo ya serikali ya umoja wa taifa nchini humo. Wabunge hao wanne walifanya mikutano Alhamisi mjini Harare na Rais Robert Mugabe na Waziri wa Fedha Tendai Biti, mjumbe wa chama cha Movement for Democratic Change - MDC.

Biti alielezea matumaini kuwa Marekani itabadili vikwazo vyake ya kiuchumi dhidi ya Zimbabwe ambavyo zimezuia misaada kwa nchi hiyo. Vikwazo hivyo pia vinapiga marufuku maafisa katika chama cha ZANU-PF cha rais Mugabe kutembelea Marekani na pia kuzuia mali zao zilizopo Marekani.

Mbunge wa chama cha Democratic Melvin Watt alisema kuondoa sehemu ya vikwazo hivyo, vinavyojulikana kama Zidera, sio kitu kitakachotokea haraka. Lakini alisema kumepatikana maendeleo kadha katika serikali ya umoja wa taifa Zimbabwe.

XS
SM
MD
LG