Rais wa Marekani Barack Obama anaadhimisha mwaka mmoja tangu aliposaini mpango wa kuchochea uchumi wa dola bilioni 787 ulioleta mabishano, akisema ulizuia hali ya kuzorota kwa uchumi kuelekea kubaya zaidi.
Katika hotuba yake ya White house leo amesema mpango huo umeokoa au kutengeneza kazi zipatazo milioni 2 na kuweka msingi wa mipango ya muda mrefu ya kukuza uchumi. Lakini wapinzani warepublikan wanasema mpango huo haufanyi kazi na umeshindwa kupunguza ukosefu wa ajira.
Mpaka hivi sasa utawala wa obama umeshatumia chini ya nusu ya hizo dola bilioni 787.
Wakosoaji wa Republikan wanasema mpango huo wa kuchochea uchumi ni sababu moja Marekani ina nakisi kubwa ya bajeti ambayo inaweza kuumiza uchumi.