Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 17, 2024 Local time: 18:30

ODM Kususia Baraza la Mawaziri Kenya


Washirika wa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga wamesema watasusia mikutano ya baraza la mawaziri mpaka mgogoro wa madaraka baina ya Waziri Mkuu na Rais Mwai Kibaki umepatiwa ufumbuzi.

Viongozi hao wawili walikwaruzana mwishoni mwa wiki baada ya Waziri Mkuu kutangaza kuwasimamisha kazi mawaziri wawili - William Ruto wa Kilimo na Prof. Sam Ongeri wa Elimu - kutokana na tuhuma za rushwa katika wizara zao, na saa chache baadaye Rais Kibaki akatangaza kuwa amefuta uamuzi huo wa Waziri Mkuu kwa sababu hakushauriwa.

Msemaji wa chama cha ODM cha Waziri Mkuu alisema Jumanne kuwa waziri mkuu huyo hawezi kufanya kazi zake vizuri katika serikali kwa sababu madaraka yake yamedhalilishwa na Rais Kibaki.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG