Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 01, 2023 Local time: 11:54

Clinton Atoka Hospitali


Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton ametolewa hospitali a mjini New York mapema leo baada ya kufanyiwa operesheni ya kupanua mshipa unaopeleka damu katika moyo wake.

Terry McAuliffe, mshauri wa karibu wa Bw Clinton, mwenye umri wa miaka 63, alithibitisha leo kuwa rais huyo wa zamani ameruhusiwa kuondoka katika hospitali ya Columbia Presbyterian. Taarifa kutoka kwa mwakilishi wa maswala ya kisheria wa Bw Clinton pia imethibitisha kutoka kwake hospitali na kusema Bw Clinton amewashukuru sana madaktari waliomshughulikia pamoja "na watu wengi waliomtumia salamu za kumtakia afueni ya haraka."

Matamshi ya madaktari yamesema Bw Clinton hakuwa na dalili zozote za kupatwa na mshtuko wa moyo isipokuwa tu mishipa inayopeleka damu katika moyo ilikuwa imeziba. Clinton alifanyiwa operesheni kubwa ya moyo miaka sita iliyopita.

Rais Barack Obama alimpigia simu bw Clinton Alhamisi jioni wakati akiwa hospitali kumjulia hali.

XS
SM
MD
LG