Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 11, 2023 Local time: 03:58

Uchaguzi kufanyika Sudan Aprili


Mahakama kuu ya Sudan imeamua wagombea wengine wawili wanaweza kushiriki kwenye uchaguzi wa Rais wa mwezi Aprili, uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia nchini humo kwa zaidi ya miongo miwili.

Mahakama hiyo iliongeza jina la Fatima Abdel Muhamed wa chama cha Sudanese Socialist Union, kwenye orodha ya wagombea siku ya Jumatatu, atakuwa ni mwanamke Sudan kugombea urais.

Mahakama pia iliongeza jina la Munir sheikh el Din Jallab wa chama cha New Democratic Nationalist kwenye orodha.

Kuna wagombea 12 wanapigania kiti cha rais akiwemo rais wa sasa Omar Al Bashir . Bw. Bashir amefunguliwa mashtaka na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita kwa mashitaka ya uhalifu wa kivita huko Darfur.

XS
SM
MD
LG