Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 22:10

Makamu Rais wa Kenya ziarani Marekani


Makamu Rais wa Kenya Stephen Kalonzo Musyoka, yuko hapa nchini Marekani kwa ziara ya siku tano. Musyoka amefuatana na spika wa bunge la Kenya Kenneth Marende.

Lengo la ziara yake ni kutoa picha nzuri ya Kenya baada ya msukosuko wa kisiasa uliogubika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, mara tu baada ya uchaguzi mkuu uliopita.

Akizungumza na wadau mbalimbali hapa Washington, Makamu Rais huyo wa Kenya, alisema Kenya haitarejea tena katika mapigano yanayochochewa na tofauti za kikabila kama ilivyoshuhudiwa wakati wa uchaguzi uliopita.

Bwana Musyoka aliiambia Sauti ya Amerika kuwa serikali inafanya kila jitihada kukabiliana na ufisadi na kuwafikisha mahakamani wale waliohusika na wizi wa fedha za msaada wa elimu ya bure kwa shule za msingi nchini Kenya.

XS
SM
MD
LG