Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 23:50

Obama Alaani Mswada wa Ushoga Uganda


Rais wa Marekani Barack Obama ameukosoa vikali mswaada wa kupinga ushoga nchini Uganda ambao endapo utapitishwa na bunge utaweka adhabu ya kifo katika baadhi ya kesi.

Akizungumza leo hapa Washington Rais Obama alisema hatua hiyo ni mbaya. Alisema kwamba japo watu hawakubaliani kuhusu ndoa za mashoga, si sahihi kuwalenga mashoga na kudidimiza ubinadamu wao.

Bwana Obama alitoa matamshi hayo wakati wa sala ya kifungua kinywa leo hapa Washington, iliyosimamiwa na kundi la uenezaji dini lijulikanalo kama The Family. Mwanasiasa mmoja wa Uganda David Bahati ambaye wanaharakati wanasema ni mwanachama wa The Family, ndiye aliyependekeza muswada huo wenye ubishani mkubwa nchini Uganda.


XS
SM
MD
LG