Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 19:09

AU wamkatalia Ghadafi mwaka mwengine


Rais wa Libya Muammar Gadhafi amkubali kuondoka kama mwenyekiti wa Umoja wa mataifa 53 ya Afrika, lakini hakukubali kuondoka bila ya kutoa maneno makali dhidi ya umoja huo. Bw. Gadhafi aliwakemea viongozi wenzake kwa kukataa kuunga mkono mpango wake wa kuunda muungano wa mataifa ya Afrika.


Kwa juu juu mkutano ulipoanza ilionekana kana kwamba mambo yalikua mazuri. Viongozi wa mataifa ya Afrika waliingia kwenye ukumbi wa mkutano, na dakika 20 baadaye walitoka na kutangaza kwamba rais wa Malawi Bingu wa Mutarika atashika zamu kama mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika kwa mwaka huu.

Lakini tangazo hilo lilificha ugomvi ulokuwepo ndani ya chumba cha mkutano, juu ya nani atachukuwa mamlaka ya umoja huo, uteshi ambao mashahidi wanasema ulikua nusra usababishe kutupiana ngumi miongoni mwa wajumbe usiku wa Jumamosi.

Kiongozi wa Libya Muamar Gadhafi alitazamia kuendelea kama mwenyekiti kwa awamu ya pili, ili kuona mpango wake wa muungano wa kisiasa na kiuchumi wa Afrika unatekelezwa. Lakini baada ya kumkabidhi kiongozi wa Malawi mamlaka ya mwenyekiti, bw Gadhafi katika hotuba yake ya kuaga, alitowa joto la roho, kwa kuwakashifu wenzake kwa ukosefu wa nia ya kisiasa.

“Si dhani tutaweza kuyabeba majukumu yanayotukabili. Si dhani kama tutaweza kukamilisha kitu muafaka katika siku zijazo kwa sababu nikizungumza kulingana na ujuzi wangu wa Umoja wa Afrika, viongozi wa bara hili wana upungufu wa uwelevu wa kisiasa na hivyo basi hawana nia ya dhati ya kisiasa.”

Bw. Gadhafi alijiita mwanajeshi wa Afrika, na kusema ataendelea na lengo lake la kuliunganisha bara hilo. Aliushambulia Umoja wa Afrika kwa kupoteza wakati kwa kutowa hotuba ndefu ndefu, maazimio, na matangazo, huku wakidharau dunia inayoendelea kubadilika.
Alisema kuna Umoja wa Ulaya ambao unabadilika na kua nchi moja na inafanyika kwa dhati.
Bw. Gadhafi alisema falau angelijuwa kuwa uwenyekiti wa AU una nguvu chache tu, basi angelikataa kuwa mwenyekiti wake.

Mwenyekiti mpya wa umoja wa Afrika rais wa Malawi, Bingu Mutarika, alisema kuwa naye pia alikubaliana na baadhi ya malamiko ya bw Gadhafi.
“Njia mbele kwa mkutano mkuu wa AU, ni kutambua kwamba Afrika sio bara masikini, bali ni watu wake walio masikini. Hebu tuzingatie kwamba Ulaya na nchi nyingi za magahribi, ziliendelea mbele kwa kutumia mbao, nyama na samaki kutoka Afrika, lakini Ulaya na nchi za magharibi hazikuendelea kwa sababu ya maazimio na matangazo. Walichukuwa hatua. Hatua thabiti Kwa hiyo na wahimiza nanyi muchukuwe hatua, na hatua ziada na ziada.”


Kwenye kikao cha ufunguzi wa mkutano wa viongozi, katibu mkiuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon pia alitoa wito wa kushughulikiwa kwa haraka masuala muhimu ya bara hilo hasa changamoto za usalama huko Sudan na Somalia. Bw Ban alitoa wito pia kwa uungaji mkono mkubwa zaidi wa kimataifa kwa serekali ya mpito ya Somalia.

XS
SM
MD
LG