Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 21, 2023 Local time: 06:49

Malecela: kuweka mihula kwa wabunge ni kukiuka Demokrasia


Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania ambaye pia ni mbunge wa siku nyingi John Malecela amesema mjadala wa kuweka ukomo kwa wabunge wa Tanzania, waachiwe wananchi ambao ndio wanajua nani anastahili kuwawakilisha.

Malecela ambaye ni miongoni mwa wabunge waliokaa kwa muda mrefu katika bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania amesema kwa ufahamu wake wa siasa za kimataifa hakuna nchi duniani inayoweka ukomo kwa wabunge kukaa madarakani akitolea mfano wa Marekani, Uingereza, Urusi na China.

Malecela amesema katika bunge la sasa la Tanzania karibu asilimia 80 ya wabunge ni vijana na haelewi kauli zinazotolewa kuwa wabunge wengi ni wazee zinatoka wapi. Aliwataka wananchi wanaozungumza hivyo kufanya utafiti wa kina badala ya kuropoka kwenye vyombo vya habari.

Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa wadau mbali mbali nchini Tanzania wakitaka kuwepo na ukomo wa kipindi cha ubunge nchini humo, ili kutoa fursa ya mawazo mapya katika bunge hilo, na hasa baada ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mizengo Pinda, kusema kuwa yeye anaona kuna umuhimu wa kuwa na ukomo wa mbunge kukaa bungeni.


XS
SM
MD
LG