Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 13:00

Marekani yasitisha msaada  Kenya


Marekani imesimamisha msaada wa dola milioni saba kwa ajili ya wizara ya elimu nchini Kenya kutokana na tuhuma za rushwa. Hatua hiyo imetangazwa leo kufuatia kupotea kwa dola milioni moja nukta tatu kutoka mpango wa kusaidia elimu ya msingi.

Balozi wa Marekani nchini Kenya Michael Ranneberger, ambaye ametangaza hatua hiyo, anasema watu wanaojihusisha na udanganyifu wanastahili kushitakiwa na kufungwa na wala si kuwafukuza kazi tu.

Mwezi desemba mwaka jana rais wa Kenya Mwai Kibaki aliiagiza tume ya kupambana na rushwa nchini humo kuchunguza kupotea kwa dola milioni moja nukta tatu.

Karibu maafisa 26 kutoka wizara ya elimu nchini Kenya wamesimamishwa kazi katika kashfa hiyo lakini hadi sasa hakuna hata mmoja aliyefikishwa mahakamani. Mwezi disemba uingereza ilisimamisha msaada kwa wizara ya elimu kutokana na kashfa hiyo.

XS
SM
MD
LG