Rais wa Marekani Barack Obama amemwita mshauri mmoja wa kuaminika kutoka kwenye kampeni yake ya 2008 ili kuweza kusaidia mikakati ya chama chake cha Democratic kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka huu wa wabunge mwezi Novemba.
Maafisa wa utawala wanasema meneja wa kampeni wa zamani David Plouffe atafanya kazi na White House na wagombea uwakilishi wa chama cha Democratic ambao wanakabiliwa na kampeni ngumu.
Wademoktrat wengi wana wasiwasi kuhusu kazi zao baada ya ushindi wa wiki iliyopita wa Mrepublikan Scott Brown wa Massachusetts. Alimshinda Mdemocrat katika uchaguzi maalum wa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Seneta Ted Kennedy Mdemocraet aliyeshikilia kiti hicho kwa karibu miaka 50.
Ushindi wa Brown unakinyima chama cha Democrat wingi wa hali ya juu katika bunge unaohitajika ili kuzuia uwezo wa republican kuzuia miswaada.