Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 11:59

Kamati ya katiba Kenya yafuta cheo cha Waziri Mkuu


Baada ya majadiliano ya zaidi ya wiki moja katika mji wa Naivasha huko Kenya, hatimaye kamati ya marekebisho ya katiba nchini humo, imekubaliana kwamba Kenya yastahili kuondoa cheo cha Waziri Mkuu na badala yake kuzingatia mfumo wa serikali unaofanana na ule wa serikali ya Marekani ambapo Rais ni kiongozi wa taifa na pia serikali.

Kamati hiyo maalumu yenye wabunge 26 imeafikiana kufutilia mbali mapendekezo yaliyokuwa yametolewa na kamati ya wataalamu wa sheria kuhusu mfumo wa serikali wenye cheo cha waziri mkuu na pia Rais ambapo wote wawili wanagawanya mamlaka ya serikali.

Wanasema mfumo wa aina hii ni hatari sana kwa sababu unaweza kuitumbukiza nchi hiyo kwenye mzozo wa kikatiba ikiwa kutazuka mvutano wa uongozi kati ya Rais na waziri Mkuu. Badala yake kamati hiyo ya Bunge imependekeza Kenya inastahili kuwa na mfumo wa serikali unaofanana na mfumo ule wa serikali ya Marekani ambapo Rais atakuwa ni kiongozi wa taifa na pia serikali. Lakini kutakuwa na taasisi mbali mbali kama vile Bunge na mahakama kuu, za kuhakikisha kwamba kiongozi wa taifa hatakiuka madaraka na wadhifa aliopewa kikatiba.

Makundi mbali mbali ya wanawake nchini humo yanapinga pendekezo la kutoa madaraka yote ya uongozi kwa Rais.


XS
SM
MD
LG