Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 07, 2023 Local time: 02:03

Mtagwa Ashindwa katika Raundi ya Pili


Bondia Rodgers Mtagwa wa Tanzania alipoteza nafasi nyingine ya kuchukua ubingwa wa dunia katika uzito wa featherweight Jumamosi Januari 23 baada ya kudondoshwa katika raundi ya pili na bingwa mtetezi Yurorkis Gamboa wa Cuba katika ukumbi wa Madison Square Garden New York.

Gamboa ambaye aliwahi kushinda medali ya dhahabu katika michezo ya Olimpiki akiwakilisha Cuba alianza pambano hilo vizuri na kumtingisha Mtwaga kwa konde lake la kwanza ambalo lilimempeleka Mtanzania huyo akiweweseka katikati ya ulingo. Mtangwa alidondoshwa chini huku zikiwa zimebaki sekunde 15 katika raundi ya kwanza.

Mtagwa aliangushwa tena katikati ya raundi ya pili kwa mfulullizo wa makonde, na muda mfupi baadaye Gamboa alimaliza kazi baada ya Mtagwa kushindwa kupata nafasi ya kumkumbatia mpinzani wake ili kujipa nafasi ya kupumua. Kabla ya pambano hilo Mtagwa aliiambia Sauti ya Amerika kuwa amejitayarisha vizuri lakini inaelekea alizidiwa kwa spidi ya mpinzani wake kutoka Cuba. Msikilize Mtagwa akizungumza na Sauti ya Amerika kabla ya pambano lake la Jumamosi.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG