Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 17, 2024 Local time: 19:34

Amnesty imetoa wito wa kutopeleka  silaha Somalia.


Kundi la Kimataifa la kutetea haki za binadam Amnesty International linasema inabidi kusitisha msaada wa kijeshi kwa serekali ya mpito ya Somalia hadi pale kuna usimamizi mkali zaidi. Amnesty inaelza kwamba, silaha zinazopelekewa serekali ya Mogadishu zinagukia pia mikononi mwa waasi na kutumiwa kutenda uhalifu wa vita.

Somalia ingali imewekewa vikwazo vya silaha, lakini kibali maalum kinaweza kutolewa na Umoja wa Mataifa ili kuagizia slaha kwa ajli ya serekali ya Somalia ambayo inashambuliwa na wanaharakati wa kislamu.

Amnesty International inasema shehena za silaha kutoka Marekani, ikiwa ni pamoja na mizinga na bunduki zina sababisha hatari ya kuongezeka kwa ukiukaji wa haki za binadam katika taifa hilo lililoharibiwa na ghasia. Mwakilishi wa Amnesty Benedicte Goderiaux anasema silaha zinazotoka nchi za magharibi zinaweza kuyafikia makundi ya wanaharakati yenye silaha.

Bi Goderiaux anasema serekali ya mpito TFG yenyewe inahusika katika ukiukaji wa haki za binadam. "Vikosi vya TFG vimehusika katika mashambulio ya kiholela dhidi ya raia, hasa mjini Mogadishu, ambako vimejibu mashambulio ya makundi yenye silaha kwa kufyetua mizinga katika maeneo ya raia," alisema.

Mkurugenzi wa miradi wa tume ya kimataifa ya kukabiliana na mizozo kwa ajili ya Pembe mwa Afrika, Ernst Jan Hogendoorn anasema itakua makosa kusitisha kusafirisha silaha. Anasema msaada wa silaha kwa serekali ya Somalia kutoka nchi za Magharibi ni muhimu kuzuia kuimarika kwa uwasi wa kundi la Al-Shabaab.


XS
SM
MD
LG