Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 13:18

Ghasia za kidini zinaendelea Nigeria


Wakazi wa mji wa Jos huko Nigeria wanasema mashambulizi yamekua yakiendelea kwa siku ya nne mfululizo katika baadhi ya maeneo ambayo hayakuathiriwa mwanzoni na mapigano katika jimbo la Plateau. Wakazi hao wanasema mapigano yaliendelea licha ya serekali kupeleka wanajeshi zaid na kutangaza amri ya kutotoka nje kwa saa 24.

Mashmabulizi yangali yanaripotiwa katika mji huo wenye mvutano mkubwa kukiwepo na mapambano kati ya magenge ya waislamu wa kabila la Hausa na wakristo wa kabila la Beroms yameenea hadi mji jirani ya Jos na vijiji vya karibu.

Mwandishi wa gazeti moja katika mji huo wa Jos, Jude Owuamanam, amesema vikosi vya usalama hadi hivi sasa vimeshindwa kudhibiti ghasia hizo nje ya mji. Akieleza hali kuwa ya ukosefu kabisa wa utawala wa kisheria.

Kundi la kutetea haki za binadamu lenye makazi yake hapa Marekani, Human Rights Watch limesema zaidi ya watu 200 wameuliwa katika mapambano hayo ya siku tatu. Hadi hivi sasa maafisa wa Nigeria wamethibitisha vifo vya watu 60 tu.

Serekali ilitangaza amri ya kutotoka nje ya masaa 24 na kuwaamrisha wanajeshi kuchukua hatua thabiti kuzuia mapigano. Makamanda wa juu wa polisi na jeshi wako huko Jos kuongoza operesheni ya usalama katika mji huo ulokumbwa na ghasia.

XS
SM
MD
LG