Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 01, 2023 Local time: 06:27

Obama awataka wabunge kua na subra


Rais Barack Obama wa Marekani amewahimiza wademocrats katika baraza la senet kumsubiri seneta mteula wa chama cha republican Scott Brown kuchukua nyadhifa zake rasmi kabla ya kuendelea na majadiliano ya pendekezo la rais la mageuzi ya mfumo wa afya.

Hupo Jumani Brown alipata ushindi usiyotarajiwa wa kiti cha senet kilichokua kinashikiliwa kwa karibu nusu karne na Marhemu Edwar Kennedy wa chama cha Democratik aliyekua kiongozi wa mageuzi ya huduma za afya hapa nchini.

Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha ABC siku ya Jumatano Rais Obama aliwahimiza wa Demokrats katika baraza lka senet kutosukuma mbele mswada wa mageuzi katika bunge, lakini badala yake kusubiri hadi Brown ameapishwa.

Brown aliongoza kampeni dhidi ya mswada wa mageuzi ya afya alipogombania kiti hicho cha Massachuset na mgombea wa Demokrat Marth Coakley. Atakua Mrepublican wa 41 katika baraza la Senet la wajumbe 100, ikimanisha wabunge walowachache watakua na uwezo wa kuzuia au kuchelewesha mswada wowote utakaopendekezwa na wa Demokrats.

XS
SM
MD
LG