Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 10:59

Obama:Clinton, Bush kuongoza juhudi Haiti


Rais Barack Obama wa Marekani amewaomba marais wa zamani George W Bush na Bill Clinton kuongoza juhudi za Marekani katika ukusanyaji wa fedha kusaidia wananchi wa Haiti baada ya maafa ya tetemeko la ardhi.

Akitokeza na marais hao wa zamani Jumamosi katika White House mjini Washington rais Obama alisema viongozi hao wamekubali kuongoza juhudi hizo kama vile ambavyo rais Bush wa kwanza na Clinton walivyoongoza juhudi za kuchangisha fedha kusaidia waathirika wa Tsunami huko Indonesia miaka kadhaa iliyopita.

Marais hao wa zamani pia walitoa matamshi machache mbele ya waandishi wa habari kusema kuwa mchango mkubwa ambao wananchi wa Marekani wanaweza kutoa kusaidia watu wa Haiti ni michango ya fedha ambazo zinahitajika kwa kiasi kikubwa kurejesha huduma muhimu kwa wananchi wa Haiti.

XS
SM
MD
LG