Ubalozi wa Marekani mjini Nairobi nchini Kenya, unasema umekataa kutoa Visa kwa mkuu wa polisi wa zamani nchini Kenya, aliyeshutumiwa kufanya ukiukwaji mbaya wa haki za binadamu.
Maafisa wanasema wamekataa kutoa Visa kwa Hussein Ali, ambaye aliripotiwa kutaka kusafiri kuelekea Los Angeles nchini Marekani, kwa shughuli za kikazi. Wanaharakati wa haki za binadamu wameifurahia taarifa hiyo.
Polisi wanashutumiwa kuhusika moja kwa moja na mauaji ya mamia ya watu yaliyotokea kwenye mapigano, ya baada ya uchaguzi mkuu wa Kenya, mwanzoni mwa mwaka 2008.