Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 13, 2024 Local time: 10:35

Mafuriko ya sababisha maafa Kenya na Tanzania


Mafuriko yaliyoenea katika sehemu mbali mbali za Kenya zimewalazimisha kiasi ya watu elfu 60 kupoteza makazi yao, na takriban watu 34 kupoteza maisha. Hadi hivi sasa serekali haijatoa taarifa rasmi kuhusiana na ya waathiriwa.

Hata hivyo kufuatana na ripoti za vyombo vya habari zaidi ya watu elfu 175 wameathirika na mafuriko katika majimbo manane ya Kenya, kuanzia Ziwa Victoria huko Magharibi hadi jimbo la pwani upande wa mashariki.

Akizungumzana Sauti ya Amerika, Lucy wamboi kutoka Narok anasema wamelazimika kukimbia makazi yao na kwenda katika jengo ambalo haliku athirika na kuna zaidi ya watu 50 katika jengo hilo.

Huko Tanzania, mvua za wiki mbili zimepelekea mafuriko yaliyoharibu kabisa usafiri wa reli kati ya Dodoma na Mwanza. Waziri wa miundo mbinu Dk Shukuru Kawambwa ameiambiua Sauti ya Amerika kwamba wizara yake inaendelea kutathmini kiwango cha hasara iliyopatikana.

Amesema usafiri katika eneo hilo la wilaya ya Kilosa utaweza kuchukua hadi miezi mitatu kabla kuanza tena huduma za kawaida. Mbali na kuharibika kwa njia kuu hiyo ya reli, Dk Kawambwa anasema mafuriko yameharibu zaidi ya daraja tatu muhimu na kutahitaji kazi kubwa ya kukarabati kabla ya hali kurudi ya kawaida.

XS
SM
MD
LG